Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wanafamilia,wananchi katika Sala ya Jeneza kumsalia marehemu Furtuna Saleh Mbamba

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali, wanafamilia na wananchi katika Sala ya Jeneza kumsalia marehemu Furtuna Saleh Mbamba, katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Marehemu Furtuna Saleh Mbamba alifariki dunia tarehe 24 Juni 2026 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Al Rahma, Kilimani. Marehemu alikuwa mke wa kwanza wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema Peponi. Amin.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here