ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amemwapisha Ndg. Mansura Mosi Kassim kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni.
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika leo Juni 24,2026, Ikulu Zanzibar na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt.Mwinyitalib Haji; Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi; viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama; viongozi wa dini pamoja na wanafamilia wa Katibu Mkuu Kiongozi.
Ndg. Mansura Mosi Kassim anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo tangu kuasisiwa kwake, akitanguliwa na Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said, ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.Kabla ya uteuzi huo uliofanyika tarehe 22 Juni 2026, Ndg. Mansura Mosi Kassim alikuwa Katibu Mkuu wa Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.





