Rais Dkt.Mwinyi atoa wito kwa taasisi za fedha nchini

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema bado yapo maeneo mengi ya ushirikiano ambayo taasisi za kifedha za ndani zinaweza kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Juni 24,2026, alipokutana na ujumbe wa Benki ya Absa Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Ndugu Obeid Laizer uliofika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.

Amesema,Serikali iko tayari kushirikiana na benki za ndani zinazoonesha dhamira ya kuunga mkono juhudi za maendeleo, hususan katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya kiuchumi na ustawi wa jamii katika sekta mbalimbali.
Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Benki ya Absa Tanzania kwa utayari wake wa kushirikiana na Serikali na kuchangia maendeleo ya Zanzibar.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali imeboresha mifumo ya kugharamia miradi ya maendeleo kwa kupanua vyanzo vya fedha zaidi ya bajeti ya kawaida, hatua inayolenga kuharakisha utekelezaji wa miradi na kuongeza ufanisi.
Ameuhakikishia uongozi wa Benki hiyo kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kifedha katika kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kupitia mikopo na mifumo mingine ya ufadhili.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Ndugu Obeid Laizer, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano inaoupatia Benki hiyo na kumpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa uongozi wake unaochochea maendeleo makubwa Zanzibar.
Vilevile, ameeleza dhamira ya Benki ya Absa Tanzania ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na uchumi wa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here