DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Tuzo Maalum kwa Benki Kuu ya Tanzania kama moja ya taasisi iliyofanya vizuri katika utoaji wa gawio kwa Serikali kwa mwaka 2026.
Tuzo hiyo imepokelewa na Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba katika hafla iliyofanyika leo Juni 30,2026 Ikulu jijini Dar es Salaam.
