Serikali itaendelea kuimarisha ustawi bora wa watoto Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema,Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha malezi, makuzi, maendeleo,ulinzi na ustawi wa watoto Zanzibar.
Ameyasema hayo leo Juni 24,2026 alipokutana na ujumbe wa Taasisi ya Big Win Philanthropy ulioongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Dkt. Kesete Admasu Adams uliofika Ikulu Zanzibar kuwasilisha Ripoti ya Utafiti wa Msingi kuhusu Hali ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto Zanzibar.

Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa,maendeleo ya mtoto ni suala mtambuka linalohitaji ushirikiano wa wizara na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, ulinzi na fursa za maendeleo.

Aidha, ameipongeza Taasisi ya Big Win Philanthropy kwa mchango wake katika kuimarisha ustawi wa watoto Zanzibar.
Vilevile, Rais Dkt. Mwinyi ameridhia ombi la kuanzishwa kwa mfumo maalumu wa kidigitali wa kufuatilia maendeleo ya watoto Zanzibar, hatua itakayosaidia kubaini changamoto na kuimarisha ufuatiliaji wa malezi, makuzi na maendeleo ya watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka minane.

Kwa upande wake, Dkt. Kesete Admasu Adams amesema Taasisi hiyo imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Zanzibar katika kuimarisha maendeleo ya watoto na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mipango mbalimbali ya ustawi wa watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here