Serikali yawakuna wabunge,waimwagia sifa marekebisho ya kodi,ushuru na bidhaa

■Wammwagia sifa Waziri wa Fedha na kwamba ameanza vizuri kazi yake

DODOMA-Wabunge wameipongeza Serikali kwa usikivu na umakini wake kwa kukubali kufanyia marekebisho baadhi ya tozo, kodi na ada mbalimbali zilizokuwa zikipendezwa kwenye Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwakanwa fedha 2026/2027 iliyopitishwa jana bungeni jijini Dodoma.
Miongoni ya maamuzi yaliyowakuna wabunge ni kuondoa nia ya kutoza ushuru wa bidhaa kwenye pikipiki (bodaboda), tozo ya shilingi kumi kwenye sukari inayozalishwa hapa nchini, na kuondoa pendekezo la kuanzisha kodi zuio kwenye mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

Awali akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha Bungeni, Dodoma, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) alisema, kuwa Serikali imefanya majadiliano ya kina na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, na kuafikiana maeneo kadhaa yaliyokuwa yanapendekezwa na Serikali katika maboresho ya kodi na tozo mbalimbali.

“Muswada huu unakusudia kurekebisha Sheria mbalimbali za kodi na zisizo za kodi kwa lengo kubadili viwango vya kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya Sheria mbalimbali za kodi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara, kuweka na kuboresha taratibu za ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali, ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hususani katika sekta za kimkakati ikijumuisha viwanda, kilimo, nishati na afya ili kuongeza tija na uzalishaji, kukuza ajira na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali,”amesema Mhe. Balozi Omar.
Amefafanua baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa niaba ya wananchi kuwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha ushuru wa bidhaa wa asilimia 20 kwenye magari yenye umri wa miaka nane, lakini hayazidi miaka kumi iliyopendekezwa kwenye Muswada hadi asilimia 18;

Kupunguza ushuru wa bidhaa wa asilimia 40 uliopendekezwa kwenye Muswada kwa magari yenye umri wa zaidi ya miaka kumi lakini hayazidi miaka ishirini, hadi asilimia 35;

Kupunguza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwa magari yenye miaka inayozidi ishirini na kuendelea uliopendekezwa kwenye Muswada kutoka asilimia 50 asilimia 40;

Kuondoa pendekezo la kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye thamani ya dau la michezo ya kubahatisha kama ilivyokuwa imependekezwa kwenye Ibara ya 9 ya Muswada;

Kuweka masharti kuhusu msamaha katika Framework Agreements baina ya Serikali na kampuni za madini, ambapo tumekubaliana na Kamati kwamba, msamaha husika hautahusisha bidhaa za mafuta, utatolewa kwenye kipindi cha ujenzi wa mradi pekee na utamaliza muda wake pale tu kampuni husika zitakapoanza uzalishaji wa madini.
Aidha, kampuni itakayotumia vibaya misamaha husika itachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kusitishiwa misamaha husika na kurejesha kodi yoyote waliyosamehewa;

Kuondoa pendekezo la kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye pikipiki kama ilivyokuwa imependekezwa kwenye Ibara ya 11(g) ya Muswada;

Kuondoa pendekezo la kutoza kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia moja (1) kwenye malipo yanayohusu mazao ya kilimo, wanyama hai, maziwa, Samaki, na mabondo kama ilivyokuwa imependekezwa kwenye Ibara ya 25 ya Muswada;

Kuondoa pendekezo la kutoza kodi kwa utaratibu wa malipo ya mkupuo kwa asilimia moja (1) katika mapato yanayotokana na mazao ya kilimo kama ilivyokuwa imependekezwa kwenye Ibara ya 28 ya Muswada;

Kupunguza kiwango cha kodi kwa walipa kodi chini ya utaratibu wa makadirio kutoka kiwango cha asilimia 4.5 kinachopendekezwa kwenye Muswada hadi asilimia 4 kwa mapato yanayoanzia shilingi 11,000,001 hadi 200,000,000;
Kuongeza wigo wa matumizi ya asilimia 5 inayotokana na mgawanyo wa mapato ya tozo ya maendeleo ya reli kutumika pia kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya uongezaji thamani;kuondoa tozo ya shilingi kumi kwa sukari inayozalishwa nchini iliyopendekezwa kupitia Muswada huu na na badala yake kuweka tozo kwa sukari inayoagizwa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here