MTWARA-Timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments (WHI) ipo katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za Watumishi ambapo Juni 28,2026 imekagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa nyumba ya Watumishi 6:1 katika Shule ya Sekondari Samia Suluhu Hassan wilayani Ruangwa, pamoja na mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi 3:1 katika Kituo cha Afya Mtandi,Masasi mkoani Mtwara.
Picha mbalimbali juu zikionesha wataalamu hao wakiendelea na ukaguzi wa utekelezaji wa miradi hiyo.






