DODOMA-Wizara ya Fedha imeungana na Wizara, Taasisi za umma pamoja na Sekta binafsi, kushiriki katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu ya Wizara katika usimamizi wa fedha za umma, ukuaji wa uchumi wa Taifa na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Kuchochea uwajibikaji jumuishi kwa maendeleo endelevu”, yanafanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma kuanzia tarehe 16-23 Juni, 2026.Wizara ya Fedha inawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, ili kupata elimu, taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara pamoja na taasisi zake, sambamba na kujionea mafanikio na maboresho yanayoendelea kutekelezwa katika sekta ya fedha na uchumi nchini.



