Waziri Kombo awasilisha Ujumbe Maalum wa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Samia kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

NEW YORK-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres, na kusisitiza dhamira ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, amani na maendeleo endelevu.
Baada ya mazungumzo yao, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) alimkabidhi Mhe. António Guterres zawadi ya kitabu kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua kuvutiwa kwa muda mrefu kwa Katibu Mkuu huyo na maono, uongozi na mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here