BRUSSELS-Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 121 wa Baraza la Mawaziri wa OACPS uliofanyika Brussels, Ubelgiji, tarehe 15–16 Julai 2026.
Mkutano huo umejadili na kukubaliana kuhusu hatua za utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa OACPS uliofanyika Malabo, Equatorial Guinea, mwezi Machi 2026.Maeneo yaliyopewa kipaumbele katika utekelezaji wa maazimio hayo ni pamoja na kuendeleza uchumi wa buluu, kuimarisha biashara na uwekezaji, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kuharakisha mageuzi ya kidijitali, kuimarisha minyororo ya thamani, na kukuza ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baina ya Nchi Wanachama 79 wa OACPS kutoka Afrika, Karibiani na Pasifiki.


