DAR-Viongozi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa viongozi waliotembelea banda hilo ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, pamoja na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Baraka Leonard.
Wakati wa ziara zao, viongozi hao walipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na wataalamu wa BoT, pamoja na kupata elimu kuhusu majukumu yake katika kusimamia sera ya fedha, kudumisha utulivu wa mfumo wa fedha na kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi nchini.
Benki Kuu inaendelea kuwakaribisha wananchi kutembelea banda lake ili kupata elimu na kufahamu kwa undani zaidi kuhusu majukumu yake, huduma na mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.









