CCM yamvulia kofia Rais Dkt.Mwinyi kwa utendaji makini

ZANZIBAR-Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitahakikisha kila lililoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2025-2030 yanatekelezwa kwa wakati,kwa viwango na ufanisi unaotegemewa.

Pia CCM imempongeza Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuhimiza ujenzi wa vituo vya kisasa vya mabasi yanayotumia nishati ya umeme.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis aliyesema kuanzia huduma za usafiri wa mabasi ya umeme, ni fakhari ilioje.

Mbeto aliutaja mradi huo utawapatia wananchi huduma za usafiri wa uhakika na ubora, katika namna ya kuboresha mfumo unaoipa haiba mpya mji wa Zanzibar.

Alisema lengo la Serikali ya CCM ni kuhakikisha vyombo vya usafiri vinavyotoka maeneo ya nje ya mji, vinaishia katika vituo vya mabasi vitakavyojengwa pembezoni mwa mji.

"Yote yalioahidiwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi za mgombea urais yanatekelezwa.Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Wakoloni wameondoka na kuviacha visiwa vikiwa hohehahe kimaendeleo,"alisema Mbeto.

Aidha,alisema chama cha CCM kitaendelea kuikumbusha serikali yake na kuhakikisha hakuna ahadi hata moja itakayoachwa pembeni

Katibu huyo Mwenzi alisema kwa taasisi dhamana yoyote itakayosimamia uendeshaji wa usafiri huo mpya ,wafuate utaratibu mpya wa utoaji huduma za usafiri ili kutoa unafuu kwa wananchi.

"Katika usafirishaji lazima kuwe na utaratibu utakaowajali wazee, wagonjwa ,walemavu na wanafunzi ili wasafiri kwa urahisi bila usumbufu,"ameeleza.

Pia,Mbeto amezitaka mamlaka zinazohusika na ujenzi wa miundombinu ya barabara,kuwa makini katika kudhibiti uvamizi wa hifadhi za barabara, ikiwemo ujenzi wa maduka na majengo mengine.

"Wananchi wote wana wajibu wa kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuitunza .Mali ya umma ni mali ya kila raia hivyo lazima zilindwe na kutunzwa,"amesisitiza Mbeto

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here