DAR-Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba, amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuimarisha misingi ya utawala wa sheria kupitia maboresho ya sera, sheria na mifumo mbalimbali ya utoaji haki, hatua zinazolenga kujenga Taifa lenye haki, amani na maendeleo endelevu.

Naibu Waziri Katimba amesema kuwa, kitabu hicho kina mchango muhimu katika taaluma ya sheria na uongozi kwa kuwa maudhui yake yanaakisi uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, haki, uwajibikaji na utawala bora.
Alisema, kitabu hicho ni rejea muhimu kwa wanataaluma, watafiti, wanafunzi wa sheria na viongozi, kwani kinaeleza kwa kina mchango wa uongozi unaozingatia sheria katika kuimarisha taasisi za Serikali, kukuza demokrasia na kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa usawa bila ubaguzi.

Mhe. Katimba alisisitiza kuwa, utawala wa sheria ni msingi wa dola ya kidemokrasia na nguzo muhimu ya maendeleo ya Taifa. Alieleza kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira yanayokuza misingi hiyo kupitia marekebisho ya sheria, sera na mifumo ya utoaji haki ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na kwa usawa kwa wananchi wote.
Aidha, alibainisha kuwa Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati kwa kuimarisha huduma za msaada wa kisheria, utoaji wa elimu ya sheria pamoja na utekelezaji wa awamu ya pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia na kuendelea kuziimarisha taasisi zinazosimamia mnyororo wa haki nchini.
Katimba amesema misingi ya utawala wa sheria haiishii katika vyombo vya utoaji haki pekee, bali inahitaji ushiriki wa wananchi, taasisi za umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali ili kujenga jamii inayozingatia haki, uwajibikaji, ushirikishwaji na utawala bora.
Wito umetolewa kwa wadau wa sekta ya sheria, taasisi za elimu ya juu, watafiti na wananchi kwa ujumla kukisoma kitabu hicho ili kupata uelewa mpana kuhusu nafasi ya utawala wa sheria katika kujenga Taifa lenye haki, amani, maridhiano na maendeleo jumuishi kwani mafanikio ya Taifa yanategemea uwepo wa mfumo imara wa sheria unaolinda haki za wananchi na kuhimiza maendeleo endelevu.
Tags
Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania
Falsafa ya Sheria ya Mama Samia
Habari
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Wizara ya Katiba na Sheria