Magazeti leo Julai 1,2026

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Maryprisca Mahundi, amezindua rasmi Mfuko wa Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi katika Jimbo la Mtwara Mjini (UWEZO Program) na kusema Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za uwezeshaji wa wanawake.
Akizungumza katika hafla hiyo Juni 30, 2026, Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali inaamini kuwa maendeleo ya Taifa hayawezi kupatikana bila kuyawezeaha makundi maalum wakiwemo wanawake na vijana.

Amesema ushiriki wa makundi maalum katika shughuli za kiuchumi ni hatua ya kujivunia na kuongeza kuwa mafanikio yatapatikana kwa makundi hayo kupatiwa mafunzo stahiki.

“Serikali inaamini kuwa maendeleo ya Taifa hayawezi kupatikana bila wananchi wake kuwa na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na hii ndiyo sababu kuwndelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake na vijana kupata fursa za kiuchumi kupitia sera na programu mbalimbali,” alisema Naibu Waziri Mahundi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here