Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetangaza nafuu kwa waajiri wenye malimbikizo ya michango kwa kuwapatia fursa ya msamaha wa tozo zitokanazo na ucheleweshaji wa michango, huku ukiwataka kuchangamkia fursa hiyo ili kupunguza mzigo wa madeni, kuimarisha uzingatiaji wa sheria na kulinda haki za wafanyakazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, alisema kuwa msamaha huo, ulioanza kutekelezwa tarehe 1 Juni 2026, utaendelea hadi 31 Desemba 2026.Bw. Mshomba alieleza kuwa tangu kuanza kwa msamaha huo, waajiri wameonyesha mwitikio chanya ambapo hadi sasa zaidi ya waajiri 6,000 wamejitokeza kutumia fursa hiyo na Mfuko umekwishakusanya zaidi ya shilingi bilioni 46 za michango tangu kuanza kwa msamaha huo tarehe 1 Juni 2026.
“Tunawasihi waajiri wote kutumia fursa hii mapema. Fedha ambazo wangezilipa kama tozo wanaweza kuzielekeza katika shughuli za uzalishaji, upanuzi wa biashara, kuongeza tija na kuboresha ustawi wa wafanyakazi,” alisema Bw. Mshomba.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo












