Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete aweka jiwe la msingi ujenzi kituo cha afya na daraja Igunga,asisitiza amani kwa maendeleo ya Taifa

NA VERONICA MWAFISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila na daraja la Nyandekwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora huku akisisitiza kuilinda amani ya nchi kwa maendeleo ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoka kukagua daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti leo tarehe 08 Julai, 2026 katika maeneo hayo, Mhe. Kikwete amesema maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na ujenzi wa daraja hilo yasingekuwepo kama kungekuwa hakuna amani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiweka jiwe la msingi katika Daraja daraja la Nyandekwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tuendelee kufanya kazi kwa bidii, tuitunze amani ya nchi yetu, tumekusanyika hapa kwasababu tuna amani hivyo tusikubali kurubuniwa kuivuruga amani ya nchi yetu,” amesisitiza.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akikagua Daraja daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri hiyo.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuweka kipaumbele katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, miundombinu, maji lengo ni kutaka wananchi wafurahie matunda ya nchi yao.
Mwonekano wa Nyuma Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kininginila kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Mwonekano wa daraja la Nyandekwa lililopo katika kata ya Nyandekwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika daraja la Nyandekwa mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Kituo hiki cha afya cha Kiningínila ni mwanzo tu, kwani mpango wa Serikali ni kujenga majengo mengi zaidi ili mpate huduma mbalimbali ikiwemo ya afya ya mama na mtoto, huduma ya meno na nyingine nyingi,” amesisitiza

Aidha, amesema katika Mkoa wa Tabora, Serikali imeajiri watumishi 2200 ikiwemo watumishi wa afya ili wananchi waweze kupata huduma za kitabibu kama ilivyo katika maeneo mengine.

Kuhusu ujenzi wa daraja la Nyandekwa, Mhe. Kikwete amesema daraja hilo litaenda kuondoa adha ya muda mrefu ya kivuko iliyokuwa ikikwamisha shughuli za maendeleo ya wakazi wa Kijiji cha Manonga na maeneo jirani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Dkt. Lucia Kafumo alipokuwa akimueleza jambo baada ya Waziri huyo kukagua Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kininginila katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri hiyo.

Amesema Mhe. Rais alitoa fedha zaidi ya milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ili kutatua changamoto ya kivuko.

Mhe. Kikwete ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Tabora inayolenga kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here