Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete aielekeza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa mradi wa maji Kaliua

NA VERONICA MWAFISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa mradi wa maji unaosuasua katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora.
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kaliua katika mkutano wa hadhara wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo mkoani Tabora, Waziri Kikwete amesema Wilaya hiyo ina changamoto kubwa ya maji na Mkandarasi amechukua muda mrefu kukamilisha mradi huo.
"Najua kuwa changamoto kubwa katika eneo hili ni pamoja na maji, Mhe. Mbunge umeeleza vizuri juu ya mradi wa maji wa Ichemba ambao ulitegemewa kutatua changamoto ya maji, maagizo yangu, hatuwezi kuwa na mradi wa miaka 15, wananchi hawa wavuja jasho wanaumia kwa kusosa maji, sisi viongozi na wasimamizi hatuwezi kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote kwa kuona ni kawaida tu, Kamanda wa TAKUKURU ninakuelekeza uchunguzi wa kina ufanyike kubaini tatizo liko wapi na likishabainika hatua za kisheria zifuate mkondo wake,"amesisitiza.

Amesema Serikali itatafuta mtu mwingine wa kumalizia mradi huo ili ukamilike na wananchi waweze kunufaika na kuongeza kuwa, ni jukumu lake na viongozi wengine wanaosimamia maeneo ya utawala kuhakikisha fedha za wananchi zinatumika vizuri na thamani yake inaonekana.
Waziri Kikwete amehitimisha ziara yake leo kwa kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Uyui, Urambo na Kaliua mkoani Tabora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here