Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufungua Msimu wa Tatu wa Mafunzo ya Bespoke kwa Mawakili wa Serikali

ARUSHA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari anatarajia kufungua Msimu wa 3 wa Mafunzo ya Bespoke kwa Mawakili wa Serikali yanayotarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.
Mafunzo haya yatafanyika kwa siku tatu, kuanzia tarehe 15 hadi 17 Julai, 2026, na yatawakutanisha Mawakili kutoka Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala za Serikali, na Mamlaka za Serikali za Mitaa (RS & LGAs) nchi nzima.

Mafunzo haya yameandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuwajengea uwezo, kuongeza tija, na kuwanoa Mawakili wa Serikali katika masuala mbalimbali ya Kisheria.

Aidha, Mawakili wa Serikali wanatakiwa kuyatumia Mafunzo hayo kama fursa ya kujifunza na katika kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji na kuendelea kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuboresha huduma za kisheria nchini.

Msimu wa 3 wa Mafunzo ya Bespoke kwa Mawakili wa Serikali umebeba kauli mbiu isemayo, Kumuweka Wakili wa Serikali katika nafasi ya Uongozi wa Sheria wa Kimkakati katika kufikia Malengo ya Dira ya Taifa 2050”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here