ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar, Mkoa wa Mjini Magharibi leo Julai 31,2026.
Baada ya Sala ya Ijumaa, Rais Dkt. Mwinyi ameshiriki Sala ya Jeneza ya marehemu Sheikh Abdullah Hamid Suleiman aliyekuwa Khatibu katika misikiti mbalimbali Zanzibar iliyosaliwa katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar.
Marehemu Sheikh Abdullah Hamid Suleiman, amefariki dunia leo Julai 31,2026 na kuzikwa kijijini kwao huko Muungoni, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.






