Rais Dkt.Samia amteua Asha Dachi Mbaruk kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Asha Dachi Mbaruk kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 14, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mbaruk anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Ayub Rioba Chacha ambaye amemaliza muda wake wa kulitumikia shirika hilo.

Kabla ya uteuzi huo, Mbaruk alikuwa akihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), nafasi aliyoshikilia kwa kipindi tofauti kabla ya kuhamia TBC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here