DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 19,2026 amepokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mheshimiwa Félix Antoine Tshisekedi, uliowasilishwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda Mhe. Floribert Anzuluni Isiloketshi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kupokea Ujumbe huo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Mhe. Floribert Isiloketshi na kumuahidi kuwa Tanzania itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu na wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa nchi zote mbili.
