ATLANTA-Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amefanya mazungumzo ya ushirikiano na uongozi wa Jiji la Atlanta, Marekani.
Mazungumzo ya pande hizo mbili yalilenga maeneo ya mpira wa miguu wa wanawake, mpira wa miguu wa vijana, utalii pamoja na ushirikiano kati ya Atlanta na majiji mengine ya Tanzania.Ziara ya Rais Karia ambaye aliambatana na Marais wa mashirikisho mengine, ilitokana na mwaliko wa Meya wa Jiji la Atlanta, Andre Dickens.

