Watuhumiwa 336 wahukumiwa kwa makosa mbalimbali Arusha

ARUSHA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema hali ya ulinzi na usalama mkoani humo ni shwari ambapo kwa kipindi cha kuanzia Juni 01, 2026 hadi sasa, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 532 wa makosa ya uhalifu na kuwafikisha mahakamani ambapo kati yao, watuhumiwa 336 walihukumiwa vifungo mbalimbali.
Akitoa taarifa hiyo leo Julai 15, 2026 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amebainisha kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ulawiti, ubakaji, dawa za kulevya na kupatikana na nyara za serikali.

SACP Masejo amesema kuwa miongoni mwa waliohukumiwa ni watuhumiwa wawili kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji, mtuhumiwa mmoja alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kulawiti huku mtuhumiwa mmoja alihukumiwa miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka.

Aidha, amebainisha kupitia operesheni dhidi ya dawa za kulevya Jeshi hilo lilifanikiwa kukamata watuhumiwa 59 wakiwa na Mirungi kilogramu 752.1, watuhumiwa 33 wakiwa na bhangi kilogramu 25.2 na mtuhumiwa mmoja akiwa na Heroin kete 09.

Pia kwa kipindi hicho walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 41 wakiwa na pombe ya moshi lita 206.5 pamoja na mitambo mitatu yakutengenezea pombe hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa operesheni hizo zinaendelea kufanyika maeneo yote katika mkoa huo, sambamba na kuchukua hatua kwa baadhi ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto bila kufuata sheria za usalama barabarani.

Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao ili sheria zichukuliwe dhidi yao, na limewapongeza wananchi wanaotoa taarifa za uhalifu hali iliyopelekea kupatikana kwa mafanikio hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here