TABORA-Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeendelea na zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita Tabora hadi Kigoma katika vijiji vya Masangalubabi cha Halmashauri ya wilaya Kigoma Ujiji na Kaseke Cha Halmashauri ya Kigoma DC.
Katika zoezi hilo, wanufaika 182, wakiwemo 69 wa Kijiji cha Masangalubabi na 113 wa Kijiji cha Kaseke, wamelipwa fidia yenye jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.4, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa SGR na kuhakikisha wananchi wanapata stahiki zao kwa mujibu wa sheria.



