Tanzania na Ghana zakubaliana kuimarisha ushirikiano

ACCRA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. John Dramani Mahama, katika Ikulu ya nchi hiyo Jubilee House, jijini Accra, Ghana, tarehe 22 Julai, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. John Dramani Mahama, baada ya kuhitimisha Ziara yake ya kikazi katika Ikulu ya nchi hiyo Jubilee House, jijini Accra, Ghana, tarehe 22 Julai, 2026.

Pamoja na mambo mengine, Rais Mhe. Dkt. Samia na Mwenyeji wake Rais Mhe. Mahama walikubaliana kuimarisha ushirikiano kwa kutekeleza kwa pamoja masuala mbalimbali ya afya.
Pia, walizungumzia ushirikiano na kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya madini ambapo kwa upande wa Ghana asilimia 60 ya uzalishaji unafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia 40 unafanywa na wachimbaji wakubwa, hali inayowanufaisha wananchi wa kawaida.
Kuhusu Biashara baina ya nchi mbili kuwa na muamko mdogo, waligusia kuendelea kuipa msukumo mkubwa na hasa baada ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kuanzisha safari katika ukanda huo wa Magharibi ambapo kumeanza kuchochea fursa mbalimbali za kiuchumi tofauti na awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here