Tanzania na IMF zajadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati

BANJUL-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Zeine Zeidane katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha SDKJ, Banjul nchini Gambia.
Ni pembezoni mwa Mikutano ya African Caucus ya Mwaka 2026, ambapo pamoja na mambo mengine, Ujumbe wa Tanzania na IMF walijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na taasisi hiyo muhimu ya fedha.

Bwana Zedaine amechukua nafasi ya mtangulizi wake, Bw. Abebe Selassie, ambaye muda wake wa kushikilia nafasi hiyo ulifikia tamati hivi karibuni.
Tanzania imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) tangu ilipojiunga na IMF tarehe 10 Septemba 1962, ambapo jumla ya ahadi ya mikopo ya IMF kwa Tanzania imefikia SDR bilioni 3.27. Kati ya kiasi hicho, portfolio hai ya sasa ni SDR bilioni 1.8.

Kwa ujumla, ushirikiano wa Tanzania na na IMF umekuwa nguzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya taifa, hususan kupitia uwekezaji katika miradi ya maendeleo na msaada wa kifedha, kiufundi na kitaalam.
Kwa upande wa Tanzania,kikao hicho kilimshirikisha pia Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here