Jaji mstaafu Msoffe atoa mada kwa Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani

■Apata pia fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo mafupi na Jaji Mkuu Masaju

DODOMA-Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe tarehe 08 Julai, 2026 ametoa mada kwa Majaji wapya tisa wa Mahakama ya Rufani wanaoendelea kupatiwa Mafunzo Elekezi ya kuwaandaa kuanza kutekeleza majukumu yao katika ngazi hiyo ya juu katika mfumo wa utoaji haki nchini.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyesimama mbele kushoto) akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe mara baada ya Jaji Msoffe kutoa Mada kwa Majaji wapya tisa wa Mahakama ya Rufani tarehe 08 Julai, 2026 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni sehemu ya Majaji wapya tisa wa Mahakama ya Rufani wanaopatiwa Mafunzo Elekezi.

Mhe. Msoffe akiwa mmoja kati ya Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ametoa mada mbili ambazo ni Haki ya Msingi dhidi ya Masharti ya Kiufundi na Maombi mbele ya Jaji mmoja wa Rufani na mbele ya Jopo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanaendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akizungumza jambo na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 08 Julai, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe (hayupo katika picha) wakati Mhe. Msoffe alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 08 Julai, 2026.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe akimsikiliza Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (hayupo katika picha) alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 08 Julai, 2026.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiagana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. January Henry Msoffe mara baada ya mazungumzo mafupi yaliyofanyika wakati Jaji Mstaafu Msoffe alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 08 Julai, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma).

Aidha, baada ya kutoa mada hizo, Jaji Mstaafu Msoffe amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Jaji Mkuu amemshukuru Mhe. Msoffe kwa kutenga muda wake na kufika kutoa mada kwa Majaji hao wapya wa Mahakama ya Rufani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here