DODOMA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amekihakikishia ushirikiano Chuo cha United African Institute of Technology (UAIT) Cha Korea Kusini katika kuendeleza mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito kupitia Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).
Ahadi hiyo imetolewa Julai 9,2026 jijini Dodoma, wakati wa kikao kati ya Naibu Katibu Mkuu na Mkuu wa Chuo cha UAIT, Prof. Chang Ki Lee.Akizungumza katika kikao hicho, Mbibo amesema ushirikiano huo utaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu wengi wazawa wenye ujuzi wa kiwango cha juu katika shughuli za uongezaji thamani wa madini ya vito, hatua itakayochangia kuongeza thamani ya rasilimali za madini na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, viongozi hao wamejadiliana fursa mbalimbali za kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya Sekta ya Madini, mafunzo ya kitaalamu na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ushindani wa sekta hiyo nchini.
Tags
Habari
Kimataifa
Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC)
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)
Wizara ya Madini Tanzania




