BoT yatangaza tarehe ya kufungua Hatifungani ya Serikali namba 695 mnada namba 3 ya miaka 25

NA DIRAMAKINI
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kufungua mnada wa Hati Fungani ya Serikali ya miaka 25, Na. 695 Mnada Na. 3 unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, 2026.
Kwa mujibu wa tangazo la BoT, hati hiyo itakomaa Februari 5, 2051 ikiwa na riba ya asilimia 13.25 kwa mwaka, huku malipo ya kuponi yakifanyika mara mbili kwa mwaka, kila Februari 5 na Agosti 5.

BoT imeeleza kuwa, riba limbikizi ni Shilingi 0.0363 kwa kila Shilingi 100, huku kiwango cha chini cha uwekezaji kikiwa Shilingi milioni moja (Sh1,000,000).

Aidha, hati hiyo inaruhusu ushiriki wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi pamoja na wakazi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here