Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) umeendelea kupanuka na sasa unatekelezwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, hatua inayoakisi mafanikio ya Serikali katika kuimarisha biashara ya mazao na bidhaa kupitia mfumo wenye uwazi, ushindani na tija.
Akizungumza jana jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Idara ya Habari – MAELEZO kuhusu utekelezaji wa shughuli za Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kwa mwaka wa fedha 2025/26 na mwelekeo wa mwaka 2026/27, Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, amesema mfumo huo umeendelea kukua kwa kasi na kuchochea biashara ya mazao na bidhaa kutoka zao moja la korosho wakati ulipoanzishwa hadi kufikia mazao na bidhaa 18 kwa sasa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















