Jela kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii

MAHAKAMA ya Mwanzo Mbeya mjini imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja (miezi 12) jela Ramadhan Rudabuka (19) DJ na Mkazi wa Patamela wilayani Chunya kwa kosa la kusambaza maudhui yasiyofaa katika mtandao wa TIKTOK.
Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini Mhe Ayubu Shirima. 

Imedaiwa kuwa, mshitakiwa alijirekodi na kusambaza maudhui yasiyofaa kwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya viongozi wa Serikali kwa lengo la kupata wafuasi wengi katika akaunti yake ya TIKTOK.

Mheshimiwa Hakimu alitoa adhabu hiyo kwa Mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia kama hiyo katika matumizi ya mitandao ya kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here