Dar es Salaam, Agosti 06, 2026-Shirika la Reli Tanzania (TRC), linapenda kuuarifu umma kuwa Kamera za CCTV zilizofungwa ndani ya mabehewa ya treni za SGR zinafanya kazi kama zilivyokusudiwa na ni sehemu muhimu ya mifumo ya usalama inayotumika ndani ya treni zetu.
Shirika linawahimiza wananchi kuendelea kutumia huduma za treni za SGR kwa kujiamini, kwani usalama wa abiria unaendelea kuwa kipaumbele cha Shirika.

