NA LWAGA MWAMBANDE (KiMPAB)
KUKU wanaofugwa katika maeneo ya Kanda ya Kati hususan Dodoma na Singida wamejijengea umaarufu mkubwa miongoni mwa walaji kutokana na ladha yao inayotajwa kuwa ya kipekee, nyama yenye mchemsho mzuri na harufu inayovutia wakati wa kupikwa.
Umaarufu huo si jambo la kupuuzwa. Kwa wafugaji, ni fursa ya kiuchumi inayoweza kugeuza ufugaji wa kuku wa kienyeji kuwa chanzo endelevu cha kipato endapo uzalishaji, afya ya kuku na masoko vitaimarishwa.
Moja ya sababu zinazoweza kuchangia ladha ya kuku wa maeneo hayo ni mfumo wa ufugaji na aina ya chakula wanachopata.
Kuku wengi wa kienyeji katika Kanda ya Kati hufugwa kwa mfumo unaowapa nafasi ya kutembea na kujitafutia chakula, huku wakila mchanganyiko wa nafaka, mbegu, mabaki ya vyakula na viumbe wadogo wanaopatikana katika mazingira yao.
Mfumo huo unaweza kufanya nyama yao kuwa na muundo tofauti na kuku wanaofugwa kwa kasi kubwa kwa ajili ya nyama, ambao mara nyingi hufikia uzito wa soko ndani ya muda mfupi.
Pia, kuku wa kienyeji kwa kawaida hukua kwa muda mrefu zaidi. Ukuaji huo wa taratibu unaweza kuhusishwa na nyama kuwa na mshikamano na ladha inayopendwa na walaji wengi.
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasisitiza kuwa, kuku mwenye ladha nzuri ni mwanzo mzuri, lakini mafanikio ya mfugaji yanategemea zaidi uwezo wa kuzalisha kwa wingi bila kushusha ubora, kudhibiti gharama, kuzuia magonjwa na kupata soko linalolipa thamani halisi ya bidhaa.
Pia, kuku wa Kanda ya Kati wanaweza kuwa zaidi ya chakula mezani, wanaweza kuwa chanzo cha ajira, kipato na biashara kubwa kwa familia za wafugaji.
Kwa hiyo, badala ya kuuza kuku kwa mazoea, wafugaji wa Dodoma na Singida waendelee kufuga, waboreshe ufugaji wao, walinde ubora wa kuku wao na watafute masoko yenye thamani ili utamu unaosifiwa na walaji ugeuke kuwa faida inayoboresha maisha yao.Endelea...
1. Kuku wa Kanda ya Kati, hapa kwetu Tanzania,
Wafugaji ni thabiti, kwa kuilisha dunia,
Vema tuunde kamati, kuku kujitangazia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
2. Hapa mikoa miwili, hapa kwetu Tanzanioa,
Ufugaji wako mbali, afya watusaidia,
Kuku halisi kamili, dawa wasiotumia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
3. Kokote hapa nchini, kuku wanatufikia,
Na tena yake thamani, kubwa sana nakwambia,
Tumeshajenga imani, sote twawakimbilia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
4. Ni Dodoma na Singida, wafugaji Tanzania,
Wafuga si kawaida, kuilisha Tanzania,
Na tena muda si muda, watasambaa dunia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
5. Hebu tembeatembea, mitaani angalia,
Watu wakichotea, lishe nzuri nakwambia,
Kuku wakiwapepea, na kisha kuwatumia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
6. Nyama ya kuku ni tamu, hilo ninakuambia,
Kila chakula ni hamu, hiyo kuweza tumia,
Vema wakiwahudumu, utamu unaingia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
7. Sasa kuna mkakati, kuku kufuatilia,
Wazidi kupanda chati, uchumi ukiingia,
Za nje na ndani noti, wafugaji wafikia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
8. Kwa ufugaji wa kuku, rahisi ninakwambia,
Uchemshe chukuchuku, kula utafurahia,
Na sherehe bila kuku, hadhi haijafikia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
9. Hongera kwa wafugaji, kuku mnatupatia,
Hebu ongeza mtaji, sisi tuzidi tumia,
Kwa sababu mahitaji, makubwa ninakwambia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
10. Hawa kuku bora sana, hapa kwetu Tanzania,
Tuwaite zuri jina, jinsi twawafagilia,
Tufuge wazidi nona, nasi tukiwatumia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
11. La kuku wa kienyeji, hadhi tunawashushia,
Hawa si wa kienyeji, bora sana nakwambia,
Hili jina tulihoji, na kujibadilishia,
Kuku wa Kanda ya Kati, nyama choma tamu sana.
12. Sema kuku wa Singida, au wa Dodoma pia,
Kinywani iwe ni ada, majina kuyatumia,
Tuwatangaze kikada, kuku wetu Tanzania,