Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Agosti 14, 2026 imepitia na kuujadili mkakati wa kuimarisha huduma za Maji, lishe, upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwenye shule za msingi na Sekondari nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Mkutano wa Nne wa Bunge unaotarajiwa kuanza Agosti 25, 2026.
Katika kikao hicho, Kamati imejadili kwa kina namna bora ya uimarishaji wa huduma za maji , upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwenye Shule za msingi na sekondari nchini, pamoja na uimarishaji wa lishe katika shule za msingi nchini.Mara baada ya kuupitia mkakati huo, Kamati kupitia Mwenyekiti wake Mhe. Florent Kyombo, katika eneo la lishe imeitaka OWM – TAMISEMI kufanya utafiti wa kina ili kuwa na takwimu halisi za lishe mashuleni, kuimarisha somo la kilimo mashuleni ili kuwapatia ujuzi wa kilimo wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kupata chakula cha kutosha mashuleni.









Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo











