DODOMA-Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo Agosti 13,2026 wameshiriki kikamilifu mjadala kuhusu “Wajibu wa Kimkakati wa Mawakili wa Serikali katika Kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050,” kupitia mafunzo ya mtandaoni yaliyotolewa na Gavana mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Prof.Florens D.Luoga.
Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa na kujenga uwezo wa Mawakili wa Serikali kuhusu nafasi yao ya kimkakati katika kuchangia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, hususan katika kuimarisha usimamizi wa Sheria, Utawala bora na Utoaji wa huduma za Kisheria kwa Serikali.
Aidha, hatua hii ni muendelezo wa jitihada za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kuhakikisha mafunzo ya mara kwa mara yanatolewa kwa watumishi ili kuongeza weledi, maarifa na ujuzi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Tags
Dira 2050
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Habari
Mawakili wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali










