KAGERA-Mkoa wa Geita umekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Kagera katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Shule ya Sekondari Nyakabango, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mwenge huo umekabidhiwa na Afisa Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati, na kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Stephen Mashauri Ndaki.
Akihitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Geita, Kiongozi wa Mbio hizo, Wazo Michael Mwang’onda, amewashukuru na kuwapongeza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Mkoa wa Geita kwa ushirikiano wao mkubwa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Aidha, amewapongeza kwa kuhakikisha amani, usalama na utulivu vinaendelea kutawala katika kipindi chote cha Mwenge wa Uhuru Mkoani Geita, hivyo kuwezesha mbio hizo kufanyika kwa usalama, amani na utulivu.














