Serikali yawekeza Shilingi bilioni 16 za pampu Ruvu Juu kuongeza uhakika wa maji Dar na Pwani

DAR-Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewekeza kiasi cha Shilingi bilioni 16 za pampu mpya nane katika Mtambo wa Uzalishaji Maji Ruvu wa Juu ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na usafirishaji wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.
Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mazingira na Maji, ikiongizwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Jackson Kiswaga (Mb), imejionea uwekezaji huo katika mtambo eneo la Mlandizi, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema,pampu sita kati ya nane tayari zimewasili, na saba zikipangwa kufungwa Ruvu Juu.
Pampu hizo zina uwezo wa kusafirisha kati ya lita milioni 1.5 hadi 2 kwa saa, ikilinganishwa na pampu za awali zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha lita 900,000 hadi milioni moja kwa saa.

Mhe. Kiswaga amesema,kamati imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha miundombinu ya maji, akibainisha kuwa kukamilika kwa ufungaji wa pampu hizo kutaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.
Ufungaji wa pampu zilizobaki unaendelea, na kazi zinafanyika kwa utaratibu unaolenga kutohatarisha huduma ya maji kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here