DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amemtaka Mkandarasi wa mradi wa Uwanja wa Mpira Dodoma kuongeza kasi ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyohitajika.
Msigwa ametoa kauli hiyo Agosti 20, 2026 wakati akikagua maendeleo ya uwanja huo ambapo ameeleza hadi sasa uwanja huo umefikia asilimia 15.Amesema kuwa, Serikali inaendelea kufuatilia kwa ukaribu ujenzi wa uwanja huo hadi utakapokamilika ili kuhakikisha unakidhi viwango vya kimataifa.
Aidha, Msigwa amewapongeza Wakandarasi na Wasimamizi wa uwanja huo kwa kazi nzuri, ambapo ameridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa.










