DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewasilisha majibu ya Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.2 wa Mwaka 2026 (The Written Laws Miscellaneous Amendments No.2 Bill, 2026) leo Agosti 18,2026 bungeni jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mhe.Hamza S.Johari ameliongoza jopo la Wataalamu wa Sheria katika kuwasilisha majibu ya Serikali kuhusiana na muswada huo.Mwandishi Mkuu wa Sheria,Bw. Onorius Njole amezitaja Sheria zinazokusudiwa kufanyiwa marekebisho ni pamoja na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura ya 283, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, Sheria ya Utathimini na Usajili wa Wathamini, Sura ya 138, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288, Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sura ya 116.
Tags
Bunge la Tanzania
Habari
Kamati ya Bunge
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali









