Mwanasheria Mkuu wa Serikali ateta na Balozi wa Marekani nchini

DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza S.Johari amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Andrew Lentz, na ujumbe wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani.
Kikao hicho kimefanyika Agosti 20, 2026 katika Ofisi Ndogo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo hayo, wamejikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo, mipango ya kimkakati ya Uwekezaji, pamoja na maeneo mengine ya ushirikiano wa pande mbili.

Pande zote mbili zimesisitiza umuhimu wa kuendeleza mazungumzo, ushirikiano wa kisheria na kitaalamu, pamoja na diplomasia endelevu katika kusukuma mbele vipaumbele vya pamoja na kukuza ubia wenye manufaa kwa Tanzania na Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here