Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanogesha bonanza la Mahakama Kuu Dar es Salaam

DAR-Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameshiriki katika Bonanza maalumu la michezo lililoandaliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na kufanyika katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam tarehe 22 Agosti, 2026.
Akizungumza wakati wa Bonanza hilo, Wakili wa Serikali Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Domina Madeli ameushukuru Uongozi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwaruhusu Watumishi kushiriki katika Bonanza hilo la Michezo.

Aidha, Bi. Madeli ameeleza kuwa ushiriki wa Watumishi katika Bonanza hilo umelenga katika kuimarisha na kuboresha ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Taasisi mbalimbali zilizoshiriki, pamoja na kuimarisha na kuboresha afya za Watumishi hao.

Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameshirikii katika michezo ya riadha, kukimbia kwenye gunia, kukuna nazi, kukimbiza kuku na mchezo wa bao.

Katika mchezo wa kukimbia kwenye gunia wanawake Bi. Honorina Mushi aliibuka mshindi wa kwanza, pia aliibuka mshindi wa tatu katika riadha mita 100.

Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam limehusisha Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali kama vile Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), TAKUKURU, Jeshi la Polisi, Magereza, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima, na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here