Rais Dkt.Mwinyi aendelea kusisitiza elimu ya dini na maadili mema kwa watoto

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa madrasa kuendelea kutoa elimu bora ya dini, sambamba na kuwajengea watoto uelewa wa mafundisho wanayopokea, maadili mema na misingi sahihi ya maisha ya Kiislamu.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 7, 2026 alipojumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti Al Aqswaa uliopo Kiboje, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema elimu ya madrasa ina nafasi kubwa katika kumjenga mtoto kielimu, kiimani na kimaadili, hivyo ni muhimu watoto wasifundishwe kusoma pekee, bali waelekezwe pia kuelewa maana na tafsiri ya mafundisho wanayojifunza.
Aidha, ameeleza umuhimu wa kuendelea kuwaandaa na kuwaendeleza walimu wa madrasa ili wawe na uwezo wa kufundisha kwa ufanisi na kuwajengea watoto uelewa mpana wa elimu ya dini wanayopokea.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa Serikali, viongozi wa dini, wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana katika kuimarisha elimu ya madrasa na kushughulikia changamoto zinazokabili taasisi hizo.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi amefungua rasmi Madrasa ya Fatma, iliyopo Kiboje Mkwajuni, na kueleza matumaini yake ya kuona madrasa hiyo ikitoa mchango mkubwa katika elimu na malezi ya watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here