Rais Dkt.Mwinyi awasili nchini Serbia kumwakilisha Rais Dkt.Samia mkutano wa NAM

BELGRADE-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili leo Agosti 30,2026 jijini Belgrade, Jamhuri ya Serbia, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Kumbukumbu ya Miaka 65 tangu kufanyika kwa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi wa Harakati za Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM).
Rais Dkt. Mwinyi amewasili akiwa ameambatana na ujumbe wake, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nikola Tesla, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Uchumi wa Jamhuri ya Serbia, Mhe. Adrijana Mesarović, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia anaiwakilisha Tanzania katika Jamhuri ya Serbia, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here