Rais Dkt.Samia aridhia kujiuzu kwa Makamu wa Rais Dkt.Emmanuel John Nchimbi

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amejiuzulu nafasi hiyo, huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akiridhia ombi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 25, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt.Moses M.Kusiluka, Rais Samia amepokea barua ya ombi la kujiuzulu kutoka kwa Makamu wa Rais Nchimbi, akieleza kuwa anatarajia kuacha nafasi hiyo kuanzia Septemba 4, 2026.

“Tarehe 25 Agosti, 2026 amepokea barua ya ombi la kujiuzulu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuanzia tarehe 04 Septemba, 2026. Mheshimiwa Rais ameridhia ombi hilo,” imeeleza taarifa hiyo.

Kujiuzulu kwa Makamu wa Rais kunafungua hatua mpya ya mchakato wa kikatiba wa kujaza nafasi hiyo katika uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi imeeleza kuwa, taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitachukuliwa, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu jina la atakayeteuliwa au muda wa uteuzi huo.

Kuondoka kwa Nchimbi katika nafasi ya Makamu wa Rais kuanzia Septemba 4 kunatarajiwa kuleta mabadiliko katika muundo wa uongozi wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati taratibu za kikatiba za kumpata mrithi wake zikianza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here