Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka amesema IAA itaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira ya kujifunzia ili kandaa watalaam mahiri na kuendana na mahitaji ya programu za kisasa hususani programu zinazohusisha matumizi makubwa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Prof. Sedoyeka amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa utoaji wa programu za Shahada ya Uhasibu na Teknolojia ya Habari (Bachelor Degree in Accountancy with IT) na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta (Bachelor Degree in Computer Science) katika Kampasi ya Babati iliyofanyika Waangw’aray Mjini Babati.
“Tunaishukuru Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) imetoa jumla ya shilingi bilioni 13.7 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala, mkataba na maabara ya TEHAMA katika Kampasi ya Babati. Sisi pia tumewekeza katika teknolojia na mkakati wetu ni madarasa yetu yote yawe smart classes (madarasa janja),” amesema.
Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa dhamira ya IAA ni wanafunzi kujifunza katika mazingira yanayowapa nafasi ya kupata maarifa, kufanya mazoezi, kubuni, kujiandaa kwa mahitaji halisi ya dunia ya kazi na kuwa kutumia maarifa kutatua changamoto halisi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
























