DODOMA-Maonesho ya Nanenane 2026 yanaendelea jiini Dodoma. Banda la TRC ni mahali sahihi kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma za reli, usafirishaji wa mizigo na abiria, pamoja na fursa za uwekezaji zilizofunguliwa na Reli ya Kisasa (SGR).
Karibu ujifunze jinsi reli inavyorahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo kwa haraka, usalama na gharama nafuu, hivyo kuwaunganisha wakulima na wafanyabiashara na masoko ya ndani na nje ya nchi.
Tunakukaribisha kutembelea banda la TRC na kujionea mchango wa reli katika kukuza kilimo na uchumi wa Taifa.
