Wananchi watakiwa kuwa karibu na Jeshi la Polisi

MOROGORO-Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji (CI), Joseph Mtenga, amewataka wananchi kuwa karibu na Jeshi la Polisi kwa kuwa ni chombo muhimu katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mtenga ameyasema hayo Agosti 28, 2026, wakati alipotembelea banda la Jeshi la Polisi katika Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika katika Viwanja vya Jamhuri, Mkoa wa Morogoro.

Amesema,Jeshi la Polisi lina jukumu kubwa katika jamii, huku akibainisha kuwa vitengo mbalimbali vinavyoshiriki katika tamasha hilo vinafanya kazi zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Ametaja baadhi ya vitengo hivyo kuwa ni Dawati la Jinsia na Watoto, Polisi Jamii pamoja na Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, ambavyo amesema vina mchango mkubwa katika kutoa huduma, elimu na ulinzi kwa jamii.

Kwa upande wake, amewahimiza wananchi kutumia fursa ya uwepo wa vitengo hivyo kuelimika na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika masuala ya usalama, ulinzi wa watoto na wanawake, pamoja na mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here