Wafanyabiashara wa Tanzania wanaoagiza bidhaa kutoka China sasa wanaweza kuwalipa wazabuni wao moja kwa moja kwa kutumia Shilingi ya Tanzania, bila kulazimika kwanza kubadilisha fedha hizo kuwa Dola za Marekani kabla ya kulipwa kwa Yuan ya China.
Huduma hiyo mpya ilikuwa miongoni mwa mada kuu katika Jukwaa la Biashara Tanzania na China lililoandaliwa na Stanbic Bank Tanzania katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Jukwaa hilo liliwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania, wawakilishi wa biashara kutoka China pamoja na taasisi mbalimbali za serikali na biashara kujadili fursa za kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.










Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










