Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje watembelea Ofisi za Ubalozi nchini India

NEW DELHI-Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaohudhuria mafunzo maalum ya diplomasia nchini India wametembelea Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini New Delhi.
Katika ziara hiyo, watumishi hao walikutana na wafanyakazi wa Ubalozi na kupata fursa ya kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini India, Mheshimiwa Anisa Mbega, pamoja na watumishi wengine wa Ubalozi.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha watumishi hao Ubalozini, Mheshimiwa Balozi Anisa Mbega alisema Ubalozi umefurahi kuwapokea watumishi wenzao kutoka Wizara na kuwapongeza kwa kupata fursa ya kushiriki mafunzo hayo maalum ya diplomasia.

Balozi Mbega alisema ana imani kuwa mafunzo waliyoyapata yamewaongezea maarifa na hivyo yatachangia kuboresha utendaji wao wa kazi na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa Wizara.
Aliishukuru Serikali ya India kwa kuitikia ombi la Wizara la kuwajengea watumishi uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa tija na ufanisi na kuongeza kuwa Ubalozi utaendelea kushirikiana na Serikali ya India ili kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na India.

Watumishi hao wa Wizara walikuwa nchini India kwa mafunzo maalum ya muda mfupi yaliyofadhiliwa na Serikali ya India na kutolewa na Chuo cha Sushma Swaraj (Sushma Swaraj Institute of Foreign Service - SSIFS), yakilenga kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara katika maeneo ya diplomasia ya kisasa, masuala ya kimataifa na kikanda, historia, mabadiliko ya kidigitali,utamaduni na sera ya mambo ya nje ya India.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here