KATAVI-Madereva wa bajaji mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo,majeruhi na hasara za mali.
Hayo yamezungumzwa Agosti 13, 2026 na Sajenti wa Polisi Jojina Luoga kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani wakati akitoa elimu ya usalama barabarani katika barabara kuu ya Mpanda-Kigoma kwa madereva hao huku akiwakumbusha kuacha tabia ya kuzidisha abiria maarufu kama “mshikaki” kitendo ambacho kinaweka maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara katika hali ya hatari.

Aidha, Sajenti Luoga amewataka madereva bajaji kuacha mwendo kasi (over speed) na kuzingatia mwendo unaotakiwa kulingana na mazingira ya barabara pia wanapaswa kuwa mfano kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
